Mchezaji wa Chelsea, Willian Borges da Silva amesema kuwa asingekuwa nasababu ya kuendelea kubaki kwenye klabu hiyo kama aliyekuwa meneja wao, Antonio Conte angesalia kwenye timu hiyo.
Maneno hayo yanadhihirisha wazi kuwa wawili hao hawapikiki chungu kimoja kwani nikweli kuwa Willian aliamua kuendelea kubaki the Blues mara baada ya Conte kutimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Maurizio Sarri mapema mwezi Julai.
Alipo ulizwa na juu ya hatma yake ndani ya Chelsea alipokuwa na Conte , Willian amesema asingekuwa na nafasi ya yeye kuendelea kuitumikia timu hiyo na badala yake angefanya maamuzi ya kuondoka.

